• Wanajeshi wa Israel waua Wapalestina 4 na kujeruhi wengine 120 Ghaza

Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wamewapiga risasi na kuwaua shahidi Wapalestina wanne na kuwajeruhi wengine 120 katika Ijumaa ya 18 ya maandamano makubwa ya amani ya 'Haki ya Kurejea' katika Ukanda wa Ghaza.

Wizara ya Afya ya Palestina imetoa taarifa na kusema miongoni mwa waliojeruhiwa ni idadi kubwa ya wanawake na watoto.

Maandamano ya amani ya 'Haki ya Kurejea' yalianza Machi 30 kwa munasaba wa 'Siku ya Ardhi' katika Ukanda wa Ghaza na yamekuwa yakifanyika kila Ijumaa .

Tokea Machi 30 hadi sasa, Wapalestina karibu 150 wameuawa shahidi katika maandamano hayo ya amani baada ya kufyatuliwa risasi na wanajeshi wa utawala katili wa Israel huku wengine karibu 16,000 wakijeruhiwa.

Nchi nyingi duniani, ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na taasisi za kimataifa zinaendelea kulaani vikali jinai hizo za utawala haramu wa Israel

Wapalestina wakitumia moshi kujaribu kuziba uono wa walenga shabaha wa Jeshi la Israel katika Ukanda wa Ghaza

Maandamano ya  'Haki ya Kurejea' yalianza kwa munasaba wa kukumbuka siku ambayo utawala ghasibu wa Israel ulipora ardhi za Wapalestina Machi 30 mwaka 1976,

Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kupora ardhi za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwa lengo la kubadilisha muundo wa kijiografia wa ardhi za jadi za Palestina ili kubadilisha muundo wa ardhi hizo na kuzipa utambulisho bandia wa Kizayuni.

Jul 21, 2018 07:15 UTC
Maoni