Jul 26, 2018 03:06 UTC
  • Israel yabomoa kituo cha watoto wa Kipalestina mashariki wa mji wa Quds

Duru za habari kutoka Palestina zimeripoti kwamba maboldoza ya utawala haramu wa Kizayuni, yamebomoa kituo cha kulelea watoto wadogo pamoja na kituo cha wanawake katika eneo la Jabal al Baba karibu na mji wa al-Eizariya, mashariki mwa mji wa Quds.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, hatua ya utawala wa Kizayuni ya kuharibu maeneo mengi ya raia wa Palestina katika eneo la Jabal al Baba, ni kutekeleza mpango wa kujenga vitongoji zaidi vya walowezi wake ndani ya mji wa Quds na kupanua vitongoji hivyo. Hii ni katika hali ambayo Jumatano ya jana utawala huo khabithi ulipitisha muswada wa kujenga nyumba 270 eneo la kusini na mshariki mwa mji wa Bethlehem. 

Hali inayowakabili Wapalestina kila siku

Aidha siku ya Jumanne  vyombo mbalimbali vya habari vya Palestina viliripoti kujiri maandamano mbele ya kituo cha kamisheni ya haki za binaadamu cha Umoja wa Mataifa mjini Gaza, yaliyokuwa na lengo la kukitaka kituo hicho kuchukua hatua za kuzuia mwenendo wa utawala huo wa kuzuia shughuli za vyombo vya habari mjini Quds, kama ambavyo pia yalitaka kuishinikiza Tel Aviv kukomesha jinai zake za kila siku dhidi ya Wapalestina. Hivi karibuni utawala wa Kizayuni ulizuia shughuli za kanali ya televisheni ya matangazo ya Quds pamoja na vyombo vingine vya habari kutokana na vyombo hivyo kurusha matangazo yanayohusiana na hali ya mambo eneo la Ukanda wa Gaza. 

Tags

Maoni