Aug 12, 2018 08:14 UTC
  • Utawala wa Kizayuni wakasirishwa na uamuzi wa Colombia wa kuitambua nchi ya Palestina

Uhusiano wa kidiplomasia wa Colombia na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umekumbwa na mgogoro kufuatia uamuzi wa serikali ya Colombia kuitambua rasmi Palestina kama nchi huru na yenye kujitawala.

Mnamo tarehe 3 Agosti aliyekuwa rais wa Colombia Juan Manuel Santos alichukua hatua kabla ya kumalizika kipindi chake cha urais ya kumwandikia barua Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Riyadh Al-Maliki kumweleza kwamba nchi yake inaitambua rasmi nchi huru ya Palestina. Uamuzi huo wa serikali ya Bogota umeukasirisha utawala haramu wa Kizayuni.

Aliyekuwa rais wa Colombia Juan Manuel Santos

Naa Ladva, mwandishi wa gazeti la Kizayuni la Haaretz amesema, viongozi wa Israel wanajihisi wamepata pigo na kudhalilika kisiasa na kiusalama kutokana na uamuzi uliotangazwa na Colombia wa kuitambua rasmi nchi ya Palestina.

Ameashiria wasiwasi waliopata viongozi wa kizayuni kwa uamuzi huo wa kushtukiza uliochukuliwa na serikali ya Bogota ambayo ni mshirika wa Israel, na kueleza kwamba uamuzi huo ni kipigo kikali kwa Israel.../

Tags

Maoni