Aug 19, 2018 15:21 UTC
  • Hizbullah kwa mara ya kwanza imezindua aina mbalimbali za makombora yake

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon kwa mara ya kwanza ilipanga kuzindua leo Jumapili sehemu ya makombora yaliyotumiwa na harakati hiyo ya muqawama wa Kiislamu kwa ajili ya kuilinda nchi hiyo katika miaka ya karibuni.

Duru za kuaminika zimearifu kuwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon leo ilipanga kuzindua makombora hayo katika bustani ya makumbusho ya Mleeta inayopatikana na katika miinuko ya Iqlim al Tuffah kusini mwa Lebanon sambamba na kuonyesha idadi kadhaa ya ndege zake zisizo na rubani. Tarehe Tatu mwezi huu pia harakati hiyo ilizionyesha katika eneo la Mleeta kusini mwa Lebanon ndege zake kadhaa zisizo na rubani katika kumbukumbu ya mwaka wa 12 wa ushindi wa harakati hiyo katika vita vya siku 33 vilivyooanzishwa na utawala wa Kizayuni.  

Wamamuqawama wa Hizbullah wakivurumisha kombora katika vita vya siku 33 baina yao na Israel mwaka 2006 

Baadhi ya ndege hizo zisizo na rubani na makombora ya Hizbullah yaliyotumika katika vita hivyo vya siku 33;  yalitumiwa pia katika oparesheni ya kuikomboa miinuko ya Arsal huko Lebanon na eneo la al Qalamoon nchini Syria na vile vile yalitumika katika oparesheni ya mwaka jana  ya kutambua maeneo yalipo makundi ya wakufurishaji huko Beqaa magharibi.  

Vita vya siku 33 kati ya jeshi la utawala wa Kizayuni na wanamuqawama wa harakati ya Hizbullah vilianza mwezi Juni mwaka 2006 na kumalizika Agosti 14 mwaka huo kwa Hizbullah kuibuka na ushindi.  Harakati hiyo ya muqawama ya Lebanon ilifanikiwa pia kukomboa sehemu ya ardhi ambayo ilikuwa ikishikiliwa kwa karibu miaka mitatu na magaidi wa kitakfiri wa harakati ya al Nusra na Daesh kufuatia oparesheni iliyofanywa ya kuikomboa miinuko ya Arsal huko Lebanon na ile ya al Qalamoon magharibi huko Syria. Oparesheni hiyo ilianza mwezi Julai mwaka jana. 

Tags

Maoni