Aug 20, 2018 14:10 UTC
  • Hamas: Mapambano na Israel yataendelea hadi Palestina ikombolewe kikamilifu

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imetangaza kuwa, falsafa ya mapambano na utawala wa Kizayuni wa Israel imejengeka katika msingi wa kufikia lengo la ukombozi wa ardhi za Palestina na kuwatimua Wazayuni maghasibu kutoka ardhi takatifu za Kiislamu na Kikristo hasa mji wa Quds na Msikiti wa Al Aqsa.

Katika taarifa iliyotoelwa leo kwa munasaba wa kuwadia mwaka wa 49 tokea kuteketezwa moto sehemu ya Msikiti wa Al Aqsa, Hamas imeongeza kuwa: "Makundi yote ya mapambano ya Palestina yana uwezo wa kuendelea na mapambano na muqawama kwa kutumia  njia na suhula zote hadi itakapokombolewa Palestina yote pamoja na mji wa Quds na pia hadi wakimbizi Wapalestina watakapopata haki ya kurejea katika ardhi zao za jadi, kuachiliwa huru wafungwa Wapalestina na kuundwa nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa ni Quds Tukufu (Jerusalem).

Katika taarifa hiyo, Hamas imesema:" Maandamano ya haki ya kurejea na kuondolewa mzingiro wa Ghaza ni kati ya ubunifu wa taifa la Palestina na hiyo Wapalestina hawatasitisha maandamano."

Tukio la kuteketezwa moto Msikiti wa Al Aqsa mwaka 1969

Ikumbukwe kuwa Agosti 21 miaka 49 iliyopita, yaani mwaka 1969 Miladia, Msikiti wa al-Aqsa Kibla cha Kwanza cha Waislamu ulihujumiwa na kuteketezwa moto na Wazayuni kwa himaya ya utawala haramu wa Israel.

Mzayuni Michael Dennis Rohan aliyeuteketeza kwa moto msikiti huo alikuwa ni Myahudi mwenye misimamo ya kuchupa mipaka.

Tags

Maoni