Sep 09, 2018 02:21 UTC
  • Mkuu wa zamani wa Mossad akiri Israel haiwezi kukabiliana na teknolojia ya makombora ya Hizbullah

Naibu Mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Utawala wa Kizayuni wa Israel, Mossad, amesema Harakati ya Hizbullah ya Lebanon hivi karibuni imepata mfumo mpya wa kuongoza makombora kwa kutegemea mfumo wa GPS na hivyo kubadilisha makombora yake kuwa yenye ustadi mkubwa.

Naftali Granot amesema Hizbullah imepata mafanikio makubwa katika uga wa makobora na kuongeza kuwa:  Katika awamu mpya ya ustawi, Hizbullah imeweza kufikia uwezo wa kuunda makombora ya hali ya juu na yenye uwezo wa kuruka masafa marefu na kulenga shabaha kwa ustadi.

Makombora ya Hizbullah

Granto ameongeza kuwa, kujiamini Hizbullah kunatokana na ushindi wake katika mapambano na magaidi wa ISIS nchini Syria.

Makamanda wa  zamani wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni wameshakiri mara kadhaa kuwa Israel haina uwezo wa kukabiliana na makombora mapya ya Hizbullah ambayo yanaweza kulenga maeneo ya kiistratijia ndani ya utawala huo.

Tags

Maoni