Sep 11, 2018 07:13 UTC
  • Palestina: Marekani ni mlinda maslahi ya Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina amesema kuhusiana na kufungwa ofisi ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) nchini Marekani kwamba hatua hiyo imethibitisha kwa mara nyingine kuwa Washington ni mwakilishi pekee wa Israel na mlinda maslahi ya utawala huo wa Kizayuni.

Waziri wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameongeza kuwa: hatua ya Marekani ya kuifunga ofisi ya PLO imethibitisha kwa mara nyingine upeo wa kujitolea nchi hiyo katika kulinda maslahi ya Israel na kuonyesha kwamba iko tayari kwa hali yoyote ile kuuhami utawala wa Tel Aviv.

Riyadh al-Maliki aidha ameitaka serikali ya Palestina iandae faili la kesi ya kuchunguza jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina na kulifikisha kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).

Jengo la ofisi ya PLO mjini Washington, Marekani

Wakati huohuo John Bolton, mshauri wa usalama wa taifa wa rais wa Marekani amesisitiza kwa mara nyingine msimamo wa nchi hiyo wa kuunga mkono sera za utawala wa Kizayuni na kueleza kwamba Washington itasimama kupinga uchunguzi wowote utakaofanywa katika mahakama ya ICC kuhusiana na siasa za Israel.

Bolton aidha ametangaza kuwa ofisi ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) nchini Marekani haitafunguliwa maadamu Wapalestina hawako tayari kufanya mazungumzo na Israel.

Mshauri huyo wa usalama wa taifa wa rais wa Marekani jana alitangaza kufungwa rasmi ofisi ya PLO mjini Washington.../

Tags

Maoni