Sep 12, 2018 01:19 UTC
  • Woga wa Jeshi la Israel kuhusu uwezo wa makombora wa Hizbullah ya Lebanon

Msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel amesema kuwa uwezo wa makombora wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon na nguvu yake ya kulenga kwa mapana katika maeneo mbalimbali ya Israel ni tishio kubwa sana.

Avichay Adraee msemaji wa jeshi la utawala haramu wa Kizayuni ameongeza kuwa makombora ya harakati ya Hizbullah ni tishio kwa Israel kutokana na makombora hayo kuwa ya kisasa na idadi yake kubwa. Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesisitiza mara kadhaa kuwa harakati hiyo itahamishia vita ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu iwapo kutajiri vita yoyote dhidi ya Lebanon. 

Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon 

Itakumbukwa kuwa Israel ililazimika kukimbia baada ya kupata kipigo kikali na hasara chungu nzima kutoka kwa wanamuqawama wa Hizbullah katika  vita vya siku 33 vilivyoanzishwa na jeshi la utawala huo mwaka 2006.

Tags

Maoni