Sep 12, 2018 07:49 UTC
  • Radiamali ya Hizbullah kwa hatua za Marekani dhidi ya Palestina

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah imesema kuwa Washington inaendeleza uadui wake dhidi ya wananchi wa Palestina kwa kustafidi na mbinu zote chafu.

Hizbullah imetangaza kuwa serikali ya Marekani inaendeleza uadui wake kwa wananchi wa Palestina lengo likiwa ni kuhitimisha kadhia ya Palestina na kuwafanya raia hao waache kupigania haki zao. Marekani inaendeleza uadui wake huo kwa wananchi wa Palestina kwa kustafidi na mbinu zote za kidhulma ikiwemo kusimamisha msaada wake wa kifedha kwa mashirika ya kibinadamu yanayowahudumia wakimbizi wa Palestina, kukata misaada yake ya kifedha kwa hospitali za mji wa Quds na kuwaweka raia hao katika mbinyo.  

Hizbullah imesisitiza kuwa kusitishwa misaada hiyo ya Marekani kwa wakimbizi wa Palestina kunaonyesha kuwa misaada ya huko nyuma ya nchi hiyo chini ya anwani ya misaada ya kibinadamu ilikuwa ya uwongo; na kusudio lake  lilikuwa ni kuathiri maamuzi ya nchi mbalimbali kwa malengo ya kikoloni.  

Harakati hiyo ya muqawama ya Lebanon imeongeza kuwa hatua hizo za Marekani zinaonyesha kuwa Washington haina rafiki na muitifaki mwingine duniani ghairi ya Israel na maslahi ya utawala huo. Serikali ya Marekani tarehe 31 Agosti  pia ilikata misaada yake ya kifedha kwa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina la Umoja wa Mataifa (UNRWA). 

Shirika la UNRWA likitoa misaada kwa wakimbizi wa Kipalestina huko nyuma 
 

 

Tags

Maoni