Sep 12, 2018 13:51 UTC
  • Utafiti: Wapalestina wengi hawana imani na Trump

Utafiti mpya uliofanywa na Kituo cha Utafiti na Sera cha Palestina umeonesha kuwa, aghalabu ya Wapalestina hawana imani na Rais Donald Trump wa Marekani na wala hawataki serikali ya Washington ijihusishe na mazungumzo ya amani ya nchi yao.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo yaliyotolewa leo Jumatano, asilimia 90 ya Wapalestina waliohojiwa wanaamini kwamba Marekani inaukingia kifua na ni mtetezi wa utawala wa Kizayuni wa Israel, huku asilimia 60 wakisema kuwa hawataki serikali ya Washingon ijihusishe kivyovyote na mazungumzo ya amani ya nchi yao.

Utafiti huo wa kituo cha Palestinian Center for Policy and Survey Research umefanyika siku chache baada ya Marekani kufunga ofisi ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina PLO mjini Washington sanjari na kuwakatia misaada wakimbizi wa Kipalestina.

Trump Mzayuni

Matokeo ya utafiti huo kwa mara nyingine tena yameonesha namna mpango wa Marekani wa eti "Muamala wa Karne" kwa ajili ya kuipatia ufumbuzi migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati umegonga mwamba.

Chuki za Wapalestina dhidi ya Trump ziliingia marhala nyingine tarehe 14 Mei, baada ya rais huyo na licha ya upinzani mkubwa kieneo na kimataifa, kutangaza kuuhamishia mji wa Quds ubalozi wa Marekani uliokuweko Tel Aviv.

 

Tags

Maoni