Sep 16, 2018 14:56 UTC
  • Wapalestina wengine wawili wauliwa shahidi na Wazayuni

Wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni leo Jumapili wamemfyatulia risasi na kumuua shahidi kijana wa Kipalestina karibu na Bayt Lahm.

Shirika la habari la IRIB limezinukuu duru za Kizayuni zikidai kuwa, kijana huyo wa Kipalestina amepigwa risasi na wanajeshi wa Israel baada ya kuwajeruhi Wazayuni wawili.

Wakati huo huo Wizara ya Afya ya Palestina imeripoti kuwa, kijana mwingine mmoja wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 16 ambaye alishiriki katika maandamano ya tarehe tatu Agosti ya kupigania haki ya kurejea makwao wakimbizi wa Palestina katika ardhi zao, amekufa shahidi leo kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel kwenye maandamano hayo huko Khan Yunus, kuisni mwa Ukanda wa Ghaza.

Wapalestina wakilia kutokana na ukatili wa kuchupa mpaka wanaofanyiwa na Israel

 

Hadi hivi sasa vijana wadogo na watoto 28 wa Kipalestina wameshauliwa shahidi na Wazayuni katika maandamano ya kupigania kurejea makwao wakimbizi wa Palestina.

Maandamano ya haki ya kurejea makwao wakimbizi wa Palestina yalianza tarehe 30 Machi mwaka huu na yamekuwa yakiendelea kila Ijumaa katika mpaka wa Ukanda wa Ghaza na maeneo mengine ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Ripoti ya Wizara ya Afya ya Palestina inaonesha kuwa, hadi hivi sasa zaidi ya Wapalestina 180 wameshauliwa shahidi kwa risasi za wanajeshi katili wa Israel na zaidi ya 19 elfu wengine wameshajeruhiwa huku hali ya baadhi ya majeruhi ikiwa ni mahututi.

Tags

Maoni