• Kaka wa Mfalme Salman wa Saudia, atoroka nchi akilalamikia siasa za Mohammad Bin Salman

Kaka wa Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia na katika kulalamikia siasa za kigeni za mfalme huyo na Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo na uingiliji wake katika vita vya Yemen, ameamua kuondoka Saudia sambamba na kuwaondoa watu wa familia yake kutoka ardhi ya nchi hiyo.

Hivi karibuni Ahmed bin Abdulaziz Al Saud ambaye pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Njdani alionekana wazi akiandamana pamoja na watu kadhaa mjini Longon, Uingereza wakilaani siasa za kigeni zinazotekelezwa na Mfalme Salman bin Abdulaziz pamoja na mwanaye Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo na kadhalika nafasi yao katika kuishambulia kijeshi Yemen. Inaelezwa kuwa, matamshi ya ukosoaji wa mwanamfalme huyo wa Saudia yaliibua hasira kali ya Mfalme Salman pamoja na Mohammad Bin Salman. Video iliyochukuliwa katika moja ya mitaa ya jiji la Londona, Uingereza inamuonyesha mwanamfalme Ahmed bin Abdulaziz Al Saud akiwambia waandamanajji, utawala wa Aal-Saud hauna uhusiano wowote na kile kinachojiri Yemen na kwamba Mfalme Salman pamoja na Mohammad Bin Salman ndio waamuzi wakuu wa vita dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Ahmed bin Abdulaziz Al Saud, ndugu wa Mfalme Salman, aliyetoroka nchi

Inaelezwa kwamba, mbali na mwanamfalme huyo, wanawafalme wengine wawili wa Saudia pia wameondoka nchi hiyo katika kulalamikia siasa mbovu za kupenda madaraka Mohammad Bin Salman. Wanaharakati wa kisiasa nchini Saudia pia wanamtaja mrithi huyo wa kiti cha ufalme kuwa chanzo cha mzozo wa Yemen kwa ajili tu ya kufikia madaraka. Katika uwanja huo, wanaharakati na wapinzani wa serikali ya Riyadh wametaka kuitishwa kura ya maoni juu ya mfumo wa kiutawala nchini Saudia, kama ambavyo wametangaza uwepo wa njama kwa ajili ya kulibadili taifa hilo kuwa utawala wa kifalme wa Salamn, badala ya mamlaka ya Aal-Saud.

Sep 17, 2018 07:56 UTC
Maoni