Sep 17, 2018 15:26 UTC
  • NATO yapeleka manowari za kijeshi katika fukwe za Syria

Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) limepeleka manowari kadhaa katika fukwe za Syria, suala ambalo ni ishara ya wazi ya uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa magaidi wanaofanya jinai na mauaji dhidi ya raia na maafisa wa serikali ya Syria.

Shirika la habari la Interfax limetangaza leo kuwa, manowari za kivita za NATO zimeonekana zikipiga doria katika maji ya karibu na Syria katika bahari ya Mediterranean Mashariki.

Manowari ya kivita ya Canada inayojulikana kwa jina la Vail De Deck, manuwari ya kushambulia kwa makombora inayojulikana kwa jina la De Reiter na manowari ya Elli ya Ugiriki ni mionogni mwa manowari za kijeshi zilizotumwa katika fukwe za Syria.

Wanajeshi wa NATO

 

Shirika hilo limeongeza kuwa, manowari za kivita za Marekani zilizoko katika Bahari ya Mediterranean zimejiweka tayari kwa mashambulizi ya wakati wowote dhidi ya Syria.

Marekani na waitifaki wake mara kwa mara wamekuwa wakitishia kuivamia na kuishambulia kijeshi Syria, hasa baada ya kushindwa njama zao za kutumia magenge ya kikatili na kigaidi kufanya jinai kubwa ndani ya Syria.

Njama kubwa inayotumiwa na nchi za Magharibi kuhalalisha mashambulizi yao dhidi ya Syria ni eti kutumia jeshi la nchi hiyo silaha za kemikali katika vita vyake vya kupambana na magaidi.

Hivi sasa Syria inajiandaa kuukomboa mkoa wa Idlib wa kaskazini mwa nchi hiyo ikiwa ndiyo ngome ya mwisho ya magaidi, lakini nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zinafanya hila za kila namna kuzuia ukombozi wa mkoa huo licha ya kwamba zenyewe nchi za Magharibi zinakiri kuwa kundi kubwa la magaidi limejikusanya Idlib hivi sasa.

Tags

Maoni