• Saudia yachukua mkopo wa dola bilioni 11 kugharimia vita dhidi ya Yemen

Wakati vita vilivyoanzishwa na Saudi Arabia dhidi ya wananchi wa Yemen vikiwa vinaendelea, Mfuko wa Kifalme wa nchi hiyo umetangaza kuwa utawala wa Riyadh umepokea mkopo wa kwanza wa kimataifa wa dola bilioni 11 kwa ajili ya kulipia deni la nchi hiyo.

Kufuatia kuchelewa uuzaji wa hisa za shirika la taifa la mafuta la Saudia, Aramco, Benki Kuu ya nchi hiyo imetangaza kupitia taarifa maalumu kwamba: Kupokewa mkopo wa kimataifa wa dola bilioni 11 itakuwa hatua ya kwanza kwa ajili ya kugharimia deni la nchi hiyo.

Kutokana na wasiwasi wa kiusalama ulionao, mnamo tarehe 22 ya mwezi uliopita wa Agosti, utawala wa Aal Saud ulisimamisha utoaji hisa za shirika la taifa la mafuta la Aramco kwenye soko la hisa la nchi hiyo.

Mbali na kusitisha mpango wa utoaji hisa za Aramco katika masoko ya ndani na nje ya nchi, utawala wa Aal Saud umewatimua pia washauri wa mpango huo wanaohusika na masuala ya fedha.

Vita dhidi ya Yemen vilivyoanzishwa na muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia, vimeisababishia nchi hiyo na muitifaki wake mkuu Imarati hasara kubwa ya fedha na roho za watu, kiasi kwamba kwa mujibu wa wataalamu, vita hivyo vinaugharimu utawala wa Aal Saud dola zisizopungua milioni mia mbili kila siku.../ 

Tags

Sep 18, 2018 14:08 UTC
Maoni