Sep 19, 2018 07:06 UTC
  • Aliyekuwa gaidi wa MKO afichua namna Saudia ilivyolipa kundi hilo tani za dhahabu

Aliyekuwa mwanachama wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Munafiqeen (MKO) amefichua kuwa Saudi Arabia ililipa genge hilo dhahabu na vito vingine vya thamani kubwa vilivyokuwa na thamani ya Dola milioni 200.

Massoud Khodabandeh, mwanachama mwandamizi wa MKO ameyafichua hayo katika mahojiano na tovuti ya habari ya Jordan ya Bawaba na kueleza kuwa, mbali na tani tatu za dhahabu, utawala wa Aal-Saud wakati mmoja ulilipa kundi hilo masanduku matatu yaliyokuwa na saa za kifahari aina ya Rolex na kitambaa cha thamani kubwa cha kufunika al Kaaba.

Katika mahojiano hayo, Khodabandeh amebainisha kuwa binafsi alishuhudia maafisa wa Saudia wakiongozwa na Mwanamfalme Turki bin Faisal Al Saud wakiwapa wanachama wa ngazi za juu wa genge hilo la kigaidi vito hivyo.

Mbali na Saudia, magaidi wa MKO wanapokea misaada mikubwa ya fedha kutoka US

Wiki iliyopita, Muhammad Javad Larijani, Katibu wa Tume ya Haki za Binadanamu ya Idara ya Mahakama ya Iran aliashiria uungaji mkono wa Uistikbari wa dunia kwa magaidi wa kitakfiri na kusema, kundi la kigaidi la Munafiqeen (MKO) ndio wale magaidi wa Daesh ambao wanatumia fedha za Saudia na kutenda jinai dhidi ya binadamu.

Hivi karibuni, Shirika la Ujasusi la Utawala wa Kizayuni wa Israel MOSSAD lilijitokeza hadharani na kukiri kuhusu ushirikiano wake na kundi la kigaidi la MKO, kupanga njama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tags

Maoni