• UN: Ghaza inakaribia kusambaratika kikamilifu, Israel inaendelea kukaidi maamuzi ya kimataifa

Mratibu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Mashariki ya Kati amekiambia kikao cha Baraza la Usalama la umoja huo kwamba eneo la Ukanda wa Ghaza huko Palestina linakaribia kusambaratika kikamilifu.

Mwaka 2006 na baada ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas kushinda uchaguzi wa Bunge la Palestina, Israel ililiwekea mzingiro wa pande zote eneo la Ukanda wa Ghaza na kuzuia kuingia eneo hilo bidhaa zote muhimu ikiwa ni pamoja na chakula, madawa, nishati, vifaa vya ujenzi. 

Nikolay Mladenov ameashiria pia ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unaoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina na kusema: Hadi saa Israel haijachukua hatua yoyote ya kutekeleza azimio nambari 2234 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Nikolay Mladenov, Mratibu wa UN katika Mashariki ya Kati

Tarehe 23 Disemba mwaka 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio nambari 2234 likiutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kusitisha haraka na kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.

Israel imekuwa ikipuuza maazimio yote ya Baraza la Usalama kutokana na kukingiwa kifua na madola ya Magharibi hususan Marekani.   

Utawala huo ukisaidiwa na Marekani unafanya mikakati ya kubadili sura na muundo wa kijiografia wa ardhi za Palestina na kuzipa sura ya Kiyahudi.

Tags

Sep 21, 2018 14:06 UTC
Maoni