Sep 22, 2018 03:04 UTC
  • Marekani yatuma wanajeshi wake katika mpaka wa Iraq na Syria

Duru za Iraq zimearifu kuwa Marekani imetuma wanajeshi wake karibu na kivuko cha al Qaim katika mpaka wa Iraq na Syria.

Habari kutoka Iraq zinasema kuwa duru moja ya kiusalama katika mkoa wa al Anbar magharibi mwa Iraq imeripoti kuwa tangu siku tatu zilizopita wanajeshi wa Marekani wanajielekeza katika mkoa wa al Anbar unaopakana na Syria. Kwa mujibu wa ripoti hiyo hadi sasa hakuna oparesheni yoyote ya kijeshi iliyofanywa katika jangwa la al Anbar. 

Wakati huo huo duru za Iraq zimearifu kuwa wapiganaji wa Hashdu Shaa'bi  yaani vikosi vya kujitolewa vya wananchi wa Iraq na makundi mengine ya kijeshi ya nchi hiyo wapo katika jangwa hilo linalopatikana katika mkoa wa al Anbar ambao wana jukumu la kuhakikisha usalama unakuwepo katika mpaka wa al Qaim. 

Wanajeshi wa Marekani wakiwa katika kivuko cha mpakani cha al Qaim huko Iraq

Wanajeshi wa Marekani walilazimika kuondoka Iraq mwaka 2011 kufuatia kushindwa kwa mara kadhaa vikosi hivyo na mwaka 2014  wakawasili tena Iraq kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Daesh. Marekani iliwasili tena Iraq huku ikiongoza muungano eti wa kimataifa dhidi ya Daesh. Wakati huo huo baada ya kusambaratishwa na kupata kipigo kikali magaidi wa Daesh huko Iraq; wananchi, vyama, shakhsia na vyombo vya habari vya Iraq vimeashiria kufutwa kisingizo cha kuwepo Iraq vikosi vya nchi ajinabi na kutaka kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini kwao. 

Tags

Maoni