Sep 23, 2018 02:41 UTC
  • Marekani imewatorosha viongozi wa DAESH (ISIS) eneo la Deir ez-Zor, Syria

Duru za kuaminika za Syria zimetangaza kuwa muungano wa kijeshi wa kimataifa unaoongozwa na Marekani wa eti kupambana na DAESH (ISIS) umewatorosha viongozi kadhaa wa kundi hilo la kigaidi na ukufurishaji katika eneo la Deir ez-Zor mashariki mwa Syria.

Duru za kuaminika katika mji wa Deir ez-Zor zimeripoti kuwa ndege kadhaa za muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani zimetua kandokando ya kijiji cha Al Muraashidah kwenye kiunga cha kusini mashariki mwa Deir ez-Zor mashariki mwa Syria, mahali liliko kundi la kigaidi la Daesh,  ambapo zimewabeba na kuwahamishia mahali kusikojulikana viongozi kadhaa kwa kundi hilo la kitakfiri.

Hapo kabla pia helikopta za Marekani ziliwahi mara kadhaa kufanya operesheni maalumu ya kijeshi kwenye kiunga cha mkoa Al Hasakah kaskazini mashariki mwa Syria ya kuwatorosha magaidi wa Daesh na kuwahamishia mahali kusikojulikana.

Magaidi wa kundi la ukufurishaji la Daesh, wanaotumia vibaya Uislamu kuhalalisha jinai zao

Hatua zilizochukuliwa na Marekani katika miaka ya karibuni za kuwaokoa na kuwatorosha magaidi wa kundi la ukufurishaji la Daesh pamoja na magaidi wa makundi mengine katika maeneo tofauti ya Iraq na Syria ni miongoni mwa sababu muhimu zaidi ambazo zimethibitisha kuwa Washington inaunga mkono kistratejia ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Tangu mwaka 2014, Marekani na waitifaki wake zimeunda muungano wa kijeshi kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Daesh lakini bila kibali cha Umoja wa Mataifa wala mashauriano na serikali ya Syria. Muungano huo hadi sasa umeshaua na kumwaga damu za raia chungu nzima wasio na hatia katika nchi za Iraq na Syria.../ 

Tags

Maoni