Sep 23, 2018 14:11 UTC
  • Wananchi na raia wa kawaida wakikimbia shambulizi la kiholela la kigaidi ambao Imarati inadai eti si la kigaidi
    Wananchi na raia wa kawaida wakikimbia shambulizi la kiholela la kigaidi ambao Imarati inadai eti si la kigaidi

Katibu wa Baraza la Kitaifa la Wairani wa Marekani linalojulikana kwa jina la NIAC amesema kuwa, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zimehusika katika shambulizi la kigaidi lililotokea jana Jumamosi katika makao makuu ya mkoa wa Khuzistan wa kusini magharibi mwa Iran.

Trita Parsi ameandika hayo katika mtandao wa Intaneti wa Middle East Eye kwamba, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zimehusika katika shambulio la jana la kigaidi lililotokea mjini Ahvaz, kusini magharibi mwa Iran.

Kwa mujibu wa  Trita Parsi, viongozi wa Saudia wana uhusiano wa karibu sana na Ikulu ya Marekani, White House, na wanaendelea na siasa zao za kuingilia masuala ya nchi nyingine za Mashariki ya Kati.

Baraza la Kitaifa la Wairani wa Marekani

 

Kwa upande wake, Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran leo amesema kuwa, balozi mdogo wa Imarati hapa Tehran ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje na kukabidhiwa malalamiko ya Tehran dhidi ya matamshi ya kejeli na ya kijuba ya mshauri wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Falme za Kiarabu.

Itakumbukwa kuwa, Abdulkhaleq Abdulla, mshauri wa mrithi wa kiti cha ufalme wa Abu Dhabi amelikejeli taifa la Iran kwa kuandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba, shambulio la jana lililopelekea kuuawa hata watoto wadogo eti lilikuwa ni shambulio la kijeshi dhidi ya shabaha za kijeshi na hivyo eti si shambulio la kigaidi.

Genge la kigaidi na la ukufurishaji la al Ahwaziyyah jana Jumamosi lilifanya shambulizi la kiholela dhidi ya wananchi waliokuwa wanaangalia gwaride la kijeshi na kuua shahidi watu 25 na kujeruhi zaidi ya 60 wengine kusini magharibi mwa Iran.

Abdulkhaleq Abdulla, mshauri wa mrithi wa kiti cha ufalme wa Abu Dhabi

Tags

Maoni