• Hashdu sh-Sha'abi yaonya juu ya njama za Marekani za kuwaingiza Iraq magaidi wa Daesh

Msemaji wa kamandi ya upande wa kaskazini ya Harakati ya Wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi ya nchini Iraq ameonya juu ya njama za Marekani za kuwasaidia magaidi wa genge la Daesh (ISIS) kutoka Idlib, Syria kuingia nchini humo.

Ali al-Husseini, amesisitiza kwamba, kuna ulazima wa kuimarishwa ulinzi katika mpaka wa Idlib kwa kufanya doria ya nchi kavu na angani. Sambamba na kubainisha kwamba, maeneo ya kaskazini mwa Iraq yako katika usalama kamili, al-Husseini ameongeza kwamba, mpaka wa Iraq na Syria unahitaji usalama zaidi na ni lazima kuwekwe vizuizi vya chuma ili kuwazuia wanachama wa kundi hilo kuingia ardhi ya Iraq.

Kundi hatari la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) ambalo baada ya kushindwa Syria linajipanga kurudi Iraq

Kwa mara kadhaa viongozi na shakhsia mbalimbali nchini Iraq wamekuwa wakitahadharisha juu ya njama chafu za Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu zenye lengo la kuwarejesha magaidi wa Daesh ndani ya nchi hiyo kwa lengo la kuchafua usalama na amani ya Iraq. Katika upande mwingine, kituo cha habari za kiusalama nchini Iraq kimetangaza kwamba, maafisa wa upelelezi na usalama nchini humo wamefanikiwa kunasa na kulisambaratisha kundi moja la kigaidi katika mkoa wa al-Anbar likiwa na kiongozi wake mkuu. Hadi sasa maafisa usalama nchini Iraq wameshanasa idadi kubwa ya mabaki ya magaidi wa genge la Daesh katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. 

Tags

Sep 25, 2018 02:24 UTC
Maoni