Oct 16, 2018 14:09 UTC
  • Netanyahu: Hivi sasa Israel ina uhusiano mzuri na nchi za Kiarabu kuliko wakati wowote

Waziri Mkuu wa Utawala Katili wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu amesema kuwa, Israel ina uhusiano wa karibu zaidi na nchi za Kiarabu kuliko wakati wowote ule.

Netanyahu, ameyasema hayo akihutubia bunge la utawala haramu wa Israel (Knesset) na kudai kuwa, vitisho vya Iran dhidi ya utawala huo, vimeifanya Tel Aviv kuwa karibu na nchi za Kiarabu. Katika miezi ya hivi karibuni, baadhi ya tawala za Kiarabu za eneo la Mashariki ya Kati, hususan utawala wa Aal-Saud zimezidisha mwenendo wa kuboresha uhusiano wao na Israel kupitia kile kinachotajwa na weledi wa mambo kuwa ni ushirikiano kwa ajili ya kupambana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Aidha juhudi za kuboresha uhusiano kati ya Israel na tawala za Kiarabu, zinafanyika katika hali ambayo, utawala haramu wa Kizayuni na kwa miaka kadhaa mbali na kufanya jinai mbalimbali dhidi ya raia madhlumu wa Palestina, pia umezikalia kwa mabavu ardhi zao ukiwemo msikiti wa al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu.

Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel mtenda jinai dhidi ya watoto wa Kiarabu

Kadhalika mgogoro wa Syria, Iraq na Yemen nayo pia chanzo chake ni utawala wa Saudia na Israel. Katika uwanja huo, Riyadh na Tel Aviv, zimekuwa zikiyaunga mkono makundi ya kigaidi nchini Syria na Iraq. Hivi karibuni pia, Noam Chomsky mwananadharia mkubwa wa Marekani alinukuliwa akisema kuwa, Iran yenye nguvu haiwezi kukubali kuziacha nchi na tawala katili ambazo zinataka kueneza uovu eneo la Mashariki ya Kati. Hii ni kusema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi kuu katika kupambana na njama chafu na hatua za mhimili wa uovu wa pande tatu za Marekani, Saudi Arabia na Israel katika eneo la Mashariki ya Kati.

Maoni