Oct 23, 2018 14:34 UTC
  • Wahka, khofu na kuchanganyikiwa baraza la mawaziri la Israel

Waziri wa Zamani wa Vita wa Utawala Haramu wa Israel, Ehud Barak amesema kuwa siasa za kupenda vita za Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo, zinaonyesha wahka, khofu na kuchanganyikiwa kwa baraza lake la mawaziri.

Ehud Barak ameyasema hayo katika mahojiano na redio ya jeshi la Israel ambapo sambamba na kuashiria kushindwa vibaya siasa za Netanyahu katika Ukanda wa Gaza ameongeza kwamba, Tel Aviv imefeli kukabiliana na muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS  kama ambavyo imeshindwa hata kuidhoofisha harakati hiyo katika Ukanda wa Gaza.

Ehud Barak, Waziri wa zamani wa Vita wa Utawala Haramu wa Israel

Kwa mujibu wa Waziri huyo wa Zamani wa Vita wa Utawala Haramu wa Israel, baraza la mawaziri la Netanyahu limeacha kuamiliana na Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na kwamba linakabiliwa na mgogoro mkubwa katika uhusiano wake na nchi ya Jordan. Ijumaa iliyopita pia, Ehud Barak alikiri kuhusika na mauaji ya Wapalestina 300. Tarehe 27 Septemba 2008, Wapalestina 225 wakiwemo wanawake na watoto na kadhalika polisi wa Palestina waliuawa katika mashambulizi ya utawala katili wa Kizayuni eneo la Ukanda wa Gaza.

Tags

Maoni