Dec 15, 2018 02:40 UTC
  • Wazayuni wakiri: Jeshi la Israel halina ubavu wa kuingia katika vita vipya

Afisa mmoja mwandamizi wa jeshi la utawala wa Kizayuni amekiri kuwa Israel haina uwezo wa kuingia kwenye vita vyengine vipya.

Katika mahojiano na gazeti la Maariv, Brigedia Jenerali Moshe Tamir, kamanda wa zamani wa jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza amekiri kuwa, jeshi la Israel haliwezi katu kuingia kwenye vita vyengine na kufafanua kwa kusema: Utendaji dhaifu wa jeshi kuhusiana na njia za chini kwa chini katika mipaka ya kaskazini umesababisha kudhoofika Israel.

Tamir ameashiria kushindwa kwa vikosi vya nchi kavu vya jeshi la Israel katika vita vya karibuni dhidi ya Ukanda wa Gaza na kutoa indhari kuhusu athari za kuendelea kuchimbwa njia za chini kwa chini na wana muqawama wa Palestina wanazotumia kwa malengo yao ya mbinu za kivita.

Wanamuqawama wa Palestina

Afisa huyo mwandamizi wa utawala wa Kizayuni wa Israel vilevile amewaomba wale wanaokosoa ripoti iliyotolewa na Meja Jenerali Yitzhak Brick, walitafakari vizuri wazo la kuanzisha vita vipya kwa kuzingatia hali ngumu inayolikabili jeshi la utawala huo haramu na akamtaka kamanda mpya wa jeshi la utawala wa Kizayuni Aviv Kochavi afikirie namna ya kutatua tatizo hilo.

Siku ya Alkhamisi, Yitzhak Brick alikiri kuwa: Jeshi la Israel halina utayari wa kuingia vitani katika mazingira ya hali ya hatari.

Kauli hiyo ya ungamo la Meja Jenerali Brick iliibua hasira na lawama za msemaji wa jeshi la Israel Ronen Manelis, ambaye kwa mtazamo wake amesema, haikupasa Brick kulitangaza jambo hilo hadharani mbele ya vyombo vya habari.../

Tags

Maoni