Dec 16, 2018 15:23 UTC
  • Netanyahu asisitiza kubomolewa nyumba za wanamuqawama wa Palestina

Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni amesistiza kubomolewa nyumba za wanamapambano wa Kipalestina ambao wiki iliyopita walishiriki kwenye oparesheni ya wanamuqawama.

Akizungumza leo mbele ya baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu amesisitiza kubomolewa nyumba za wanamapambano wa Kipalestina na kueleza kuwa wanajeshi wa Israel jana walibomoa nyumba ya familia ya Abu Hamid katika kambi ya al Am'ari huko Ramalllah katikati ya Ukingo wa magharibi mwa mto Jordan. Umu Nassir Abu Hamid mama wa shahidi mmoja na mateka sita wa Kipalestina ambaye wanawe sita wamefungwa kifungo cha maisha katika jela za Israel amesisitiza kuwa kitendo cha kubomoa nyumba za raia wa Kipalestina kitawatia hamasa zaidi Wapalestina wote ya kuzidisha mapambano na kusimama kidete dhidi ya maghasibu wa Kizayuni. Nyumba ya familia ya Abu Hamid imebomolewa mara tatu hadi hivi sasa. 

Nyumba ya familia ya Abu Hamid iliyobomolewa na Israel

Wanamapambano wa Kiislamu wa Palestina wiki iliyopita walifanya oparesheni kadhaa dhidi ya utawala wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan; ambapo katika moja ya oparesheni hizo wanajeshi watatu wa Israel waliangamizwa na mwingine mmoja kujeruhiwa vibaya.  

 

Maoni