Dec 16, 2018 15:29 UTC
  • Hamas yaadhimisha kuanzishwa kwake kwa kuzindua makombora mapya

Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, Hamas, imeadhimisha mwaka wa 31 tokea kuanzishwa kwake kwa kuzindua makombora mapya katika Ukanda wa Ghaza.

Hamas ilianzishwa mwaka 1987 punde baada ya kuanza Intifadha ya kwanza ya Wapalestina kuupinga utawala haramu wa Israel unaokalia ardhi za Palestina kwa mabavu. Harakati ya Hamas imefanya gwaride kubwa kwa munasaba huo siku ya Jumamosi ambapo Tawi la Kijeshi la Hamas, Brigedi za Izzuddin al Qassam zimeonyesha silaha zao mpya za kujihami.

Hafla hiyo imefanyika Jumamosi katika mji wa Khan Yunis katika Ukanda wa Ghaza na kuhudhuriwa na makumi ya maelfu ya Wapalestina. Sherehe za  maadhimisho ya kuanzishwa Hamas zimeendelea leo na zinafanyika katika maeneo mbali mbali ya Ukanda wa Ghaza. 

Wapiganaji wa Brigedi za Izzudin Qassam Tawi la Kijeshi la Hamas

Sherehe hizo zimefanyika siku chache baada ya wapiganaji wa Hamas kuwaangamiza Wazayuni wawili kwa kuwafyatulia risasi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, chini ya masaa 24 baada ya jeshi katili la Israel kuwaua shahidi Wapalestina watatu, wakiwamo wanachama wawili wa harakati hiyo.

 

Tags

Maoni