Dec 17, 2018 09:33 UTC
  • Qatar kuwajengea makazi wakimbizi wa Yemen

Mfuko wa Maendeleo wa Qatar ambayo ni taasisi ya masuala ya kibinadamu ya nchi hiyo pamoja na Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa zimesaini makubaliano ya kujenga makazi kwa ajili ya raia elfu 26 wa Yemen waliokimbia vita vya miaka minne nchini mwao.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo yaliyosainiwa mwishoni kwa kikao cha Doha kati ya Sheikh Muhammad bin Abdulrahman Aal Thani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar na Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa makazi hayo yatajengwa Yemen kwa bajeti ya dola milioni tatu. Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataigfa imeeleza kuwa raia wa Yemen milioni mbili wamekuwa wakimbizi tangu mwanzoni mwa uvamizi wa kijeshi wa Saudi Arabia huko Yemen mwaka 2015.  

Maelfu ya raia wasio na hatia wameuawa na mamilioni ya wengine wamelazimika kuwa wakimbizi nchini Yemen kutokana na mashambulizi ya Saudi Arabia na washirika wake.   

Mkutano wa siku mbili uliomaliza kazi zake jana huko Doha mji mkuu wa Qatar ambao umeojadili hali ya usalama, amani, upatanishi, ustawi wa kiuchumi, mielekeo na mapendekezo umehudhuriwa na shakhsia watajika wa kimataifa.

Tags

Maoni