Jan 19, 2019 15:34 UTC
  • Mwanahistoria Mzayuni: Hadi miaka 30 ijayo Israel itakuwa imeshatoweka

Benny Morris, mwanahistoria mashuhuri wa Kizayuni amesema: Hadi miaka 30 ijayo Israel haitakuwepo tena, na Wazayuni watageuka kuwa jamii ndogo ya wachache.

Akizungumza katika mahojiano na gazeti la Kizayuni la Haaretz, Morris ameongeza kuwa, Israel itadhoofika na kufifia, na Wazayuni, ambao ni jamii ya wachache, wataghariki ndani ya bahari pana ya Palestina; na katika miaka 30 hadi 40 ijayo, Waarabu watawazidi Wazayuni.

Benny Morris, ambaye ametumia muda wa miaka tisa katika kituo cha taaluma za Mashariki ya Kati cha Chuo Kikuu cha Ben-Gurion kufanya utafiti hadi kufikia tathmini yake mpya aliyotoa hivi karibuni, anaitakidi kwamba, Wapalestina hawatoachana na malengo yao matukufu ya kuhakikisha wanazitwaa ardhi zao zote zinazokaliwa kwa mabavu na wala suluhu haitofikiwa kwa msingi wa kugawana ardhi, kwa sababu Wapalestina wamedhamiria kufikia lengo lao tukufu la kuidhibiti ardhi yao yote inayokaliwa kwa mabavu na kuwatokomeza Wazayuni.

Wapalestina wanaendeleza Intifadha dhidi ya utawala wa Kizayuni hadi ushindi

Mwanahistoria huyo wa Kizayuni amebainisha pia kwamba, katika hali ya sasa Waarabu wengi zaidi wanaishi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kulinganisha na Wazayuni, na katika hali isiyoweza kuepukika, eneo hilo lote linaendelea kugeuka kuwa nchi ambayo, akthari ya watu wake ni Wapalestina; na Wazayuni wataendelea kuwa jamii ndogo ya walio wachache miongoni mwa Waarabu ambapo hatimaye watakimbilia Marekani na Magharibi.

Morris amesisitiza kwamba: Israel haitodumu; na Wapalestina ndio watakaoshinda, ambapo katika miaka 30 hadi 50 ijayo watawazidi na kuwashinda Wazayuni.../

Tags

Maoni