Feb 23, 2019 03:45 UTC
  • Baba yake Hoda Muthana awasilisha mashtaka rasmi dhidi ya serikali ya Marekani

Baba wa binti Hoda Muthana ambaye alikuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la Daesh huko Syria amewasilisha rasmi malalamiko yake kwa serikali ya Marekani.

Ahmed Ali Muthana, baba yake Hoda, binti mwanachama wa kundi la kigaidi la Daesh ameiomba mahakama  mjini Washington iidhinishe utambulisho na uraia wa binti yake na imruhusu yeye kurejea Marekani na mwanaye. 

Bila ya kuashiria hatua za White House ya kuasisi na kuyaunga mkono makundi ya kigaidi, Rais Donald Trump wa Marekani amemuagiza Mike Pompeo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo kutomruhusu Hoda Muthana kurudi Marekani. Hata hivyo wakili anayemtetea binti huyo mwanachama wa zamani wa kundi la Daesh amesema kuwa Hoda Muthana ni mzaliwa wa New Jersey kaskazini mashariki mwa Marekani. Mike Pompeo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani pia ametoa taarifa akisema kuwa Hoda Muthana si Mmarekani na hana kigezo chochote cha kisheria cha kufanya safari Marekani.

Huda Muthana miaka minne iliyopita aliondoka Marekani na kuelekea Syria. Familia ya binti huyo inasema kuwa, mtoto wao amezaliwa Marekani na kwamba anapasa kuruhusiwa kurejea nchini humo pamoja na mwanaye mwenye umri wa wa miezi 18. Anasena anajuta kuondoka marekani na kujiunga na kundi hilo la kigaidi na yuko tayari kwenda mahakamani kutokana na kushirikiana na kundi hilo.

Hoda Muthana akiwa na mwanaye wa kiume wa miezi 18 

Serikali ya Marekani na nchi za Ulaya waitifaki wa Washington waliyafadhili na kuyanga mkono makundi ya kigaidi huko Syria na Iraq. 

Tags

Maoni