Mar 19, 2019 06:47 UTC
  • Hizbullah ya Lebanon: Oparesheni ya Silfit ni dhihirisho la uwezo wa wanamapambano wa Palestina

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon (Hizbullah) imeitaja oparesheni iliyofanywa na wanamuqawama wa Palestina dhidi ya Wazayuni huko Silfit kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni liwa ni nukta adhimu katika maendeleo ya muqawama na ni ishara ya uwezo wa wanamuqawama hao mbele ya jinai za Israel.

Itakumbukuwa kuwa wanajeshi watatu wa Israel waliuawa katika oparesheni iliyofanywa na wanamuqawama wa Palestina juzi Jumapili huko Silfit katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Aidha walowezi sita wa Kiyahudi walijeruhiwa katika oparesheni hiyo. 

Wanajeshi wa Israel wakiwa katika hofu baada ya wenzao kuuawa 

Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon jana Jumatatu ilitoa taarifa na kueleza kuwa oparesheni ya Silfit ni ishara ya ubunifu wa wanamuqawama wa Palestina na kwamba wanamapambano hao kwa kuchagua mahali na wakati mwafaka wa kutekeleza operesheni hiyo wamethibitisha kuwa chokochoko zinazozidi kushtadi za Israel dhidi ya Wapalestina, kamwe hazitasalia bila ya jibu.  

Harakati ya Hizbullah imepongeza pia oparesheni ya ushindi ya Wapalestina huko Silfit na kumpongeza pia mwanamuqawama aliyetekeleza oparesheni hiyo ya kishujaa  na kuongeza kuwa: Mwanamuqawama huyo ameonyesha kuwa kijana wa Kipalestina anatumia mbinu na shuhula zozote zinazowezekana ili kukomboa ardhi yake.

Tags

Maoni