Mar 20, 2019 16:17 UTC
  • Zaidi ya askari 70 wa muungano vamizi wa Saudia wameangamizwa kwa kombora la Wayemen

Katika shambulizi la kombora lililotekelezwa jana usiku na jeshi la Yemen kwa kushirikiana na muqawama wa wananchi kuelekea kusini magharibi mwa Saudia, zaidi ya askari 70 wa muungano vamizi unaoongozwa na Saudia, wameangamizwa.

Mtandao wa habari wa Al-Masirah umemnukuu mmoja wa viongozi wa jeshi la Yemen akisema kuwa makumi ya askari wa muungano vamizi unaoongozwa na Saudia wakiwemo makamanda na maafisa wa ngazi ya juu jeshini, wameangamizwa au kujeruhiwa katika shambulio la kombora lililotekelezwa dhidi ya eneo la Al-Khaubah, la mkoa wa Jizan. Kabla ya hapo pia kikosi cha mizinga cha jeshi la Yemen kilitekeleza shambulizi la makombora ya balestiki ya aina ya Badr 1 dhidi ya ngome za wavamizi wa Saudia katika eneo la Al-Khaubah na miinuko ya al-Nar ya mkoa wa Jizan.

Harakati ya wananchi ya Answarullah ambayo imekuwa ikitoa kipigo kikali kwa wavamizi wa Saudia 

Kadhalika jeshi la Yemen limefanikiwa kudhibiti ngome kadhaa za askari wa Saudia katika eneo la Al-Talaa na mkoa wa Najran, kusini mwa Saudia. Wakati huo huo Mohammed Ali al-Houthi, Mkuu wa Baraza Kuu la Mapinduzi nchini Yemen amesema, kuwa na uhusiano mwema wa pande mbili na majirani na pia dunia ni chaguo pekee na nukta ya kuanza mazungumzo na amesisitiza kwamba, malengo ya kuizingira Yemen kamwe hayatotimia kwa upande wowote. Ali al-Houthi ameyasema hayo katika ujumbe alioutuma kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Tags

Maoni