Mar 24, 2019 15:17 UTC
  • Russia, Syria na Human Rights Watch wakanusha madai ya Trump kuhusu ISIS

Russia, Syria na Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch wamepinga madai ya rais wa Marekani, Donald Trump ya kwamba magaidi wa Daesh (ISIS) wameshasambaratishwa kikamilifu katika nchi za Iraq na Syria.

Televisheni ya al Alam imetangaza habari hiyo na kuinukuu serikali ya Russia ikisema kuwa, madai ya Trump kuhusu kusambaratishwa kikamilifu magaidi wa Daesh hayana ukweli kwani kwa mujibu wa tathmini tofauti, hivi sasa bado kuna maelfu ya magaidi wa genge hilo nchini Syria.

Kwa upande wake, Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch limekanusha haraka madai hayo ya Trump na kusisitiza kuwa, bado magaidi wa ISIS wako nchini Syria na hata mashariki au magharibi mwa Mto Furat.

Nayo serikali ya Syria imesema kuwa, bado magaidi wa Daesh wako nchini humo na kwamba ni askari wa Syria ndio wanaopambana na magaidi hao, si Marekani na washirika wake.

Mwanajeshi wa Syria akifurahia ushindi baada ya kutimuliwa magaidi wa Daesh (ISIS) na wengineo katika kambi ya Wapalestina ya Yarmouk

 

Donald Trump amedai kuwa Marekani na washirika wake wamewasafisha magaidi wa Daesh katika kona zote za Syria na Iraq.

Rais huyo wa Marekani aidha ametoa maneno ya kuchekesha alipodai kuwa, serikali yake itaendelea kuwa macho katika kukabiliana na vitisho vinavyotoka kwa mabaki ya magaidi hao.

Mgogoro wa Syria ulianzishwa kwa makusudi na maadui wa taifa hilo la Kiarabu mwaka 2011 kwa kumiminwa magaidi kutoka kila kona ya dunia waliofanya jinai kubwa dhidi ya raia na maafisa wa serikali ya Syria. Mgogoro wa Iraq ulipamba moto mwaka 2014 baada ya magaidi wa Daesh wanaoungwa mkono na Marekani na waitifaki wake kuteka eneo kubwa la nchi hiyo kabla ya kufurushwa.

Tags

Maoni