Apr 22, 2019 13:56 UTC
  • Kundi la Daesh (ISIS) latangaza kuhusika na shambulizi mjini Riyadh, Saudia

Kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) limetangaza kuhusika na shambulizi dhidi ya kituo kimoja cha polisi huko Riyadh, mji mkuu wa Saudia.

Taarifa iliyochapishwa na mtandao wa habari wa kundi la Amaq imesema kuwa, shambulizi hilo la jana lilifanywa na watu wanne wanachama wa genge hilo kwenye kituo hicho cha polisi.

Hii ni katika hali ambayo jana vyombo vya habari nchini Saudia vilitangaza kuwa watu wanne wenye silaha walifanya hujuma hiyo dhidi ya kituo hicho cha usalama kwenye eneo la Az Zulfi, kaskazini mwa mji wa Riyadh na kuua watu wanne.

Maafisa usalama wa Saudia

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maafisa wa Saudi Arabia waliwaua washambuliaji wote wanne, huku polisi wengine watatu wa nchi hiyo wakijeruhiwa.

Inafaa kuashiria kuwa, baadhi ya wanachama wa kundi hilo la Daesh (ISIS) wamekuwa wakiikosoa vikali serikali ya Saudia kwa kuwa na uhusiano mkubwa na Marekani na baadhi ya tawala za kitwaghuti na kwa mara kadhaa wamekuwa wakitishia kufanya mashambulizi dhidi ya nchi hiyo inayoongozwa na mfumo wa kifalme. 

Tags

Maoni