• Qassemi:

  Qassemi: "Mfumo wa mabadilishano ya fedha baina ya Iran na Ulaya" unafuatiliwa

  Dec 03, 2018 15:39

  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Mfumo maalumu kwa ajili ya mabadilishano ya fedha kati ya Iran na Ulaya kwa kifupi SPV ungali unaendelea kufuatiliwa; na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeshabainisha wazi mategemeo iliyonayo katika suala hilo.

 • Sisitizo la EU la kuhifadhiwa ushirikiano wake wa kiuchumi na Iran

  Sisitizo la EU la kuhifadhiwa ushirikiano wake wa kiuchumi na Iran

  Nov 30, 2018 07:27

  Umoja wa Ulaya mara kwa mara umekuwa ukisisitizia haja ya kuimarishwa uhusiano wake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na sababu kuu ni nafasi muhimu na bora ya Iran katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwa ni pamoja na nafasi yake bora katika upande wa jiopolitiki, kisiasa, kiuchumi na kinishati. Jambo jingine linalopewa umuhimu na Umoja wa Ulaya ni kulinda mapatano ya nyukilia ya JCPOA.

 • Jitihada za ulaya za kulinda mapatano ya nyuklia ya JCPOA

  Jitihada za ulaya za kulinda mapatano ya nyuklia ya JCPOA

  Nov 29, 2018 03:05

  Mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji, JCPOA, ambayo yalifikiwa Julai mwaka 2015 baina ya Iran na kundi la 5+1 yalikuwa mapatano muhimu sana katika uga wa kulinda amani na usalama wa kimataifa.

 • Iran na EU zasisitizia haja ya kuendelea kufungamana na JCPOA

  Iran na EU zasisitizia haja ya kuendelea kufungamana na JCPOA

  Nov 28, 2018 07:42

  Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Umoja wa Ulaya kwa mara nyingine tena zimesema kuwa pande mbili hizo zitaendelea kuheshimu na kufungamana na makubaliano ya nyuklia ya Vienna, licha ya Marekani kujiondoa kwenye mapatano hayo ya kimataifa.

 • Ufaransa na Ujerumani kuwa wenyeji wa mfumo wa ubadilishanaji fedha na Iran

  Ufaransa na Ujerumani kuwa wenyeji wa mfumo wa ubadilishanaji fedha na Iran

  Nov 27, 2018 07:56

  Wanadiplomasia wa ngazi za juu wa Ulaya wameliambia gazeti la Wall Street Journal kuwa huenda Ufaransa na Ujerumani zikawa wenyeji wa mfumo maalumu wa ubadilishanaji fedha na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unaojulikana kama SPV, kwa shabaha ya kukwepa vikwazo vya Marekani dhidi ya Tehran.

 • Iran ina haki ya kurutubuisha tena urani kama jibu kwa Marekani

  Iran ina haki ya kurutubuisha tena urani kama jibu kwa Marekani

  Nov 25, 2018 08:18

  Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tehran ina haki ya kuimarisha urutubishaji urani katika vituo vyake vya nyuklia, kama radiamali kwa hatua ya Marekani ya kujiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

 • Sisitizo la Umoja wa Ulaya na Uturuki la kuendelea kushirikiana na Iran

  Sisitizo la Umoja wa Ulaya na Uturuki la kuendelea kushirikiana na Iran

  Nov 24, 2018 11:48

  Hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump ya kuiondoa nchi hiyo katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuiwekea tena Iran vikwazo imepingwa vikali na nchi nyingine wanachama wa makubaliano hayo ya JCPOA yaani kundi la 4+1.

 • Mapatano ya JCPOA yanatosha; Iran haitozungumza tena na Marekani

  Mapatano ya JCPOA yanatosha; Iran haitozungumza tena na Marekani

  Nov 24, 2018 02:44

  Dk. Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu juhudi za Marekani za kutaka kuanzisha mazungumzo mapya na Iran kwa kusema kuwa, mapatano yaliyofikiwa ya JCPOA ni makubaliano mazuri na kwamba Iran haitofanya tena mazungumzo na Marekani kuhusu miradi yake ya nyuklia.

 • IAEA yasisitiza tena kuwa Iran imefungamana na JCPOA

  IAEA yasisitiza tena kuwa Iran imefungamana na JCPOA

  Nov 23, 2018 07:59

  Kwa mara nyingine tena, Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) umethibitisha kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetekeleza majukumu na ahadi zake zote chini ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

 • Rais Rouhani: Iran haitasalimu amri mbele ya Marekani

  Rais Rouhani: Iran haitasalimu amri mbele ya Marekani

  Nov 19, 2018 15:55

  Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa hili litabakia kuwa huru na lenye mamlaka yake na katu halitasalimu amri mbele ya Marekani.