Jun 10, 2017 15:58 UTC
  • Marekani yaunga mkono waziwazi ISIS; Mbunge wa Congress asema: Mashambulizi ya kigaidi ya Tehran ni kwa manufaa ya Marekani

Mbunge wa jimbo la California katika Baraza la Congress la Marekani ametoa matamshi ya kijuba na kuunga mkono waziwazi mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na genge la wakufurishaji la Daesh mjini Tehran, Iran, Jumatano asubuhi.

Shirika la habari la habari la Fars limemnukuu Dana Rohrabacher, akisema hayo siku ya Alkhamisi katika kikao cha kamati ya masuala ya kigeni cha Baraza la Congress la Marekani na kusema hadharani bila ya haya kwamba, amefurahishwa na mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea mjini Tehran siku ya Jumatano. Vile vile amesema kwa kusisitiza kuwa mashambulio hayo ni kwa manufaa ya Marekani.

Dana Rohrabacher, mbunge mwenye chuki za kidini katika Baraza la Congress la Mareani

 

Jumatano asubuhi, magaidi wa Daesh walishambulia jengo la kiidara la Bunge la Iran na Haram ya Imam Khomeini, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuua shahidi raia 17 na kujeruhi wengine 52. Magaidi wote waliangamizwa mara moja na vikosi vya ulinzi vya Iran. Hadi hivi sasa makumi ya magaidi wengine wameshatiwa mbaroni katika maeneo tofauti ya Iran.

Kitendo cha mbunge huyo wa Marekani cha kuunga mkono hadharani mashambulizi ya kigaidi ya Daesh mjini Tehran kimefanyika katika hali ambayo viongozi wengi duniani na taasisi za kieneo na kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika AU zimelaani vikali mashambulizi hayo ya kikatili.

Kabla ya hapo, rais wa Marekani Donald Trump aliwakejeli wahanga wa mashambulio hayo ya kigaidi ya mjini Tehran na kuandika kwenye mtandao wake wa Tweeter kwamba eti Iran imerejelewa na shari yake yenyewe. 

Tags

Maoni