• Afisa wa zamani wa CIA:

Afisa wa zamani wa Shirika Kuu la Kijasusi la Marekani CIA amefichua kuwa shirika hilo lilihusika katika hujuma za Septemba 11 mwaka 2011.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya yournewswire.com, Malcom Howard afisa wa zamani wa CIA ambaye ni mataalamu wa uhandisi na kutokana na kuwa aliwahi kufanya kazi za kubomoa nyumba,  alitakiwa na wakuu wa CIA kushiriki katika mradi wa kuyabomoa majengo pacha ya World Trade Centre mjini New York. Howard ambaye pia alipata utaalamu wa mada za milipuko akiwa CIA mapema muongo wa 1980 anasema alikuwa miongoni mwa walioshiriki katika mradi wa kubomoa majengo pacha ya New York katika siku ambayo ni maarufu kama 9/11.

Howard ambaye alihudumia CIA kwa muda wa miaka 36 anasema wakati akifanya kazi katika shirika hilo hawakutakiwa kuuliza sababu ya mradi huo kwani walidhani ni kwa maslahi ya taifa. Howard amesema ameamua kutoboa siri hiyo baada ya kufahamishwa na madaktari kuwa hana muda mrefu wa kuishi.

Malcolm Howard

Hadi sasa kuna nyaraka nyingi ambazo zimetolewa zinazoonyesha majengo pacha ya Kituo cha Kimataifa cha Biashara (WTC) yalivyoporomoka kwa njia iliyoratibiwa kpitia mada za miripuko na wala hayakuporomoka kutokana na kugongwa na ndege mbili za abiria kama inavyotangazwa rasmi.

Ikulu ya White House imekataa kutoa ripoti kamili ya matukio ya siku hiyo kwa sababu ripoti hiyo inaashiria ushiriki wa Saudi Arabia katika mradi huo wa CIA. Kundi la al Qaeda lilidai kuhusika na hujuma hizo za 9/11.

Jul 16, 2017 04:14 UTC
Maoni