• Naibu Spika wa Ujerumani: Erdogan anataka kuiendesha Uturuki kidikteta

Naibu Spika wa Bunge la Ujerumani amesema kuwa Rais wa Uturuki anataka kuiendesha nchi hiyo kidikteta na kwa msingi huo amesema Ujerumani inapasa kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Ankara.

Bi Claudia Roth Naibu Spika wa Bnge la Shirikisho la Ujerumani amesisistiza kuwa Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ameazimia kuanzisha utawala wa kidikteta nchini humo na kwa msingi huo ameitaka serikali ya Ujerumani iwaunge mkono wapinzani wa serikali ya Ankara. 

Bi Roth ameashiria namna asilimia karibu 50 ya wananchi wa Uturuki walivyopinga marekebisho ya katiba yaliyopendekezwa na Erdogan katika kura ya maoni iliyofanyika nchini humo na kueleza kuwa wapinzani wa Erdogan wanataka kupatikana anga iliyo wazi na ya kidemokrasia nchini humo. Ameongeza kuwa, wapinzani hao wanapaswa kuungwa mkono. Wakati huo huo Naibu Spika huyo wa Bunge la Shirikisho la Ujerumani ametaka kusitishwa haraka uuzaji wa bidhaa na misaada ya kiuchumi ya Ujerumani kwa Uturuki.

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki 

Uhusiano kati ya Berlin na Ankara umeathiriwa na mivutano kufuatia kutiwa mbaroni nchini Uturuki waandishi habari kadhaa wa Ujerumani na baada ya Berlin kukubali ombi la kuwapa hifadhi baadhi ya wanajeshi wa Uturuki na pia kufuatia hotuba iliyotolewa na viongozi wa Ujerumani mbele ya hadhara ya raia wa Uturuki kabla ya kufanyika kura ya maoni hivi karibuni nchini Uturuki.  

Tags

Jul 17, 2017 07:14 UTC
Maoni