• Madai ya uhusiano wa nyuklia wa Iran na Korea Kaskazini; kelele mpya kuhusu shughuli za nyuklia za Iran

Afisa mmoja wa serikali ya Uingereza amedia kuwa Iran imeisaidia Korea Kaskazini kuimarisha uwezo wake wa silaha za nyuklia.

Gazeti la Sunday Telegraph katika toleo lake la Jumapili limemnukulu afisa wa ngazi za juu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza ambaye hakutaka jina lake litajwe akisema kuwa: "Korea imeweza kuimarisha uwezo wake wa silaha za nyuklia kutokana na uungaji mkono wa kisiri wa Iran." Afisa huyo  amedai kuwa: "Ni vigumu kuwaamini (Wakorea Kaskazini) kuwa wametegemea uwezo wao katika kujiimarisha kinyuklia."

Gazeti la Sunday Telegraph limeendelea kudai kuwa mbali na Iran, Russia pia inashukiwa kutoa msaada na kushirkiana na Korea Kaskazini katika miradi yake ya silaha za nyuklia.

Madai kama hayo pia yaliwahi kutolewa huko nyuma lakini kwa muundo mwingine. Miaka minne iliyopita yaani mwaka 2013, wakati mazungumzo ya nyuklia ya Iran yakiwa yanaendelea, baadhi ya duru za habari na kidiplomasia zilidai kuwa jaribio la nyuklia la Korea Kaskaizni kwa kutumia urani iliyorutubishwa lilifanyika kwa msaada na ushirikiano wa Iran. Madai hayo yalitolewa pasina kuwepo ushahidi wowote.

Kombora la Korea Kaskazini katika maonyesho ya kijeshi

Wakati huo, gazeti la Wall Street Journal lilimnukulu afisa wa zamani katika serikali ya rais Barack Obama akisema: "Marekani ina wasi wasi kuhusu shughuli za nyuklia za Korea Kaskazini na ushirikiano wake na Iran."

Gazeti hilo lilimaliza kwa kuandika kuwa, Iran haiwezi kuunda bomu la atomiki kwa siri na kuandika: "Serikali ya Korea Kaskazini inadai ina vichwa vya silaha za nyuklia ambavyo vinaweza kubebwa na makombora yake ya masafa ya wastani." 

Mfano mwingine wa madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran ni kutangazwa ripoti bandia kuhusu uwezekano wa kuwepo shughuli za kinyuklia zenye malengo ya kijeshi nchini Iran katika eneo la Parchin.

Iran imepinga madai hayo na hata imewaruhusu wakaguzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA kutembelea eneo hilo na wakala huo umetoa ripoti iliyotangaza rasmi kuwa madai hayo hayana msingi.

Kudai kuwa kuna ushirikiano wa kisiri baina ya Iran na Korea Kaskazini katika uga wa nyuklia na makombora ni madai ambayo yanalenga kuhalalisha uchochezi na uibuaji mgogoro wa Marekani katika Rasi ya Korea. Kuhusiana na hilo, sasa Marekani inataka kudai kuwa inaingilia masuala ya eneo hilo kutokana na wasiwasi wa kuhusika Iran na Russia katika mradi wa silaha za nyuklia wa Korea Kaskazini.

Image Caption

 

Hii ni katika hali ambayo, sababu kuu ya Korea Kaskazini kuchukua hatua zisizo za kawaida na hivyo kuibua mgogoro katika Rasi ya Korea, ni tisho la Marekani na waitifakie wake wa kieneo dhidi ya Pyongyang.

Marekani haijatekeleza ahadi zake ilizotoa kwa Korea Kaskazini baada ya mazungumzo ya pande sita bali Washington imezidisha vitisho na vikwazo dhidi ya nchi hiyo.

Hatua ya Korea Kaskazini kuendeleza majaribio ya nyuklia inatokana na mwenendo wa kutoaminika Marekani. Pamoja na hayo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa ikisisitiza kuhusu kufungamana nchi zote na mkakataba wa NPT wa kuzuia utegenezaji na usambazaji wa silaha za nyuklia na kwamba umiliki wa silaha za nyuklia ni tishio kwa usalama wa dunia nzima.

Sep 11, 2017 11:26 UTC
Maoni