• Wafanyakazi wa White House wachoshwa na upunguwani wa Trump

Wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani, White House wasema kuwa wamechoshwa na matatizo ya kiakili na upunguwani wa rais wa nchi hiyo, Donald Trump.

Ukurasa wa Intaneti wa gazeti la Independent la nchini Uingereza umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani wamemfananisha Trump na sufuria la mapishi ya haraka ambalo linaweza kuripuka wakati wowote.

Maafisa wa White House wamesema kuwa, mara zote Trump ni mtu wa hasira na asiyesarifika hususan katika siku za hivi karibuni ambapo amelemewa na lawama hasa kutokana na namna alivyoamiliana na mgogoro wa Puerto Rico na mgogoro wa Bob Corker, seneta wa ngazi za juu wa chama chake cha Republican ambaye amemlaumu Trump kwa kuilekeza Marekani upande wa Vita vya Tatu vya Dunia.

Ikulu ya Marekani White House

 

Gazeti la Independent la nchini Uingereza limeongeza kuwa, watu wa karibu na Trump katika ikulu ya White House  wanasema kuwa, rais huyo wa Marekani amechoshwa na lawama na malumbano yasiyoisha ya maneno.

Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti hilo, uhusiano wa Trump na John Kelly, Mkuu wa Wafanyakazi wa White House ulitegemewa urejeshe nidhamu katika Ofisi ya Rais wa Marekani ambayo imekumbwa na madhara yasiyolipizika.

Kabla ya hapo Gregory Meeks, mjumbe wa kamati ya uhusiano wa nje ya bunge la Marekani alikuwa ameiambia televisheni ya CNN kwamba, Donald Trump haheshimu cheo chake cha urais bali anafanya mambo kama mtoto mdogo. 

Oct 12, 2017 02:48 UTC
Maoni