• Marekani, Israel zatengwa kimataifa baada ya kujiondoa UNESCO

Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zimetengwa kimataifa bada ya kutangaza kujiondoa katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amebainisha masikitiko yake baada ya Marekani kutangaza kujiondoa UNESCO. Utawala wa rais wa Marekani Donald Trump jana Alkhamisi ulitangaza kujiondoa katika taasisi hiyo ya kimataifa kulalamikia misimamo yake iliyo dhidi ya Israel.

Utawala haramu wa Israel nao pia umetangaza kujiondoa UNESCO na kudai kuwa eti taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa ni eneo la sarakasi.

Wakati huo huo mwenyekiti wa UNESCO anayemaliza muda wake, Irina Bokova amesema, ni wazi kuwa UNESCO haikuwa muhimu kwa Marekani. Amesema ni jambo la kusikitisha kuwa katika wakati huu ambapo dunia imekumbwa na migogoro mingi, Marekani imeamua kujiondoa katika taasisi ya Umoja wa Mataifa iliyojikita katika kuimarisha elimu, amani na kulinda utamaduni.

Msikiti wa al-Aqsa

Nazo China na Russia zimekosoa uamuzi wa Marekani wa kujiondoa UNESCO na kusema zinaiunga mkono taasisi hiyo ya kimataifa.

Mwaka uliopita, uamuzi wa UNESCO wa kusisitiza kuwa Mayahudi hawana uhusiano wowote na Masjidul Aqsa, ambacho ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu, wala mji wa Quds, uliwakasirisha sana viongozi wa utawala wa Kizayuni na Marekani. UNESCO pia imelaani vitendo vya Wazayuni vya kupotosha asili ya kihistoria ya Quds na maamuzi hayo yamewachukiza sana Wazayuni na watawala wa Marekani.

Oct 13, 2017 14:56 UTC
Maoni