Hotuba iliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani na misimamo yake ya kustaajabisha kuhusu sekta ya ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimezusha tufani na kimbunga kikubwa.

Hata hivyo inaonekana kuwa, kimbunga na tufani hiyo imemshtua na kumsomba rais huyo mwanagenzi na asiye na tajiriba wa Marekani kwani katika kipindi kifupi baada ya hotuba yake jamii ya kimataifa ilirudisha mapigo makali zaidi na kumshambulia.

Baada tu ya hotuba ya Doland Trump, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Dakta Hassan Rouhani alitoa majibu madhubuti na kurudisha mapigo kwa kiongozi huyo. Waziri wa zamani wa Marekani, Madeleine Albright alimjibu Trump kwa kusema: Kudhoofisha makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 kunaiweka hatarini Marekani na kuifanya itengwe na waitifaki wake. Albright amesisitiza kuwa, hotuba ya Trump ilijaa ghadhabu na ni hatari kubwa. 

Madeleine Albright

Wakati huo huo kiongozi wa chama cha Green nchini Marekani, Jill Ellen ameashiria hotuba ya Rais wa nchi hiyo Donald Trump kuhusu makubaliano ya nyukllia ya JCPOA na kusema: "CIA ilipindua serikali ya kidemokrasia ya Iran hapo mwaka 1953 na badala yake ikamsimika madarakani dikteta hatari. Iran na mataifa mengine hayataki vita. Mataifa hayo yanaitaka Marekani isiingilie masuala yao", mwisho wa kunukuu. 

Baada ya hotuba ya Trump dhidi ya Iran Ijumaa iliyopita maneno ya "IRGC" yaani Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, "Rouhani" na "JCPOA" zilikuwa miongoni mwa hastagi zilizotia fora katika mtandao wa kijamii wa twetter. 

Rais Hassan Rouhani

Seneta maarufu wa chama cha Democratic Dianne Feinstein katika jimbo la California ametoa majibu makali dhidi ya Trump na kusema kuwa, misimamo yake kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA itaisababishia matatizo Marekani. Feinstein amesema: Kwa msimamo hii ya Trump kuhusu makubaliano ya JCPOA inatupasa kutafakari kwa kina kuhusu usalama wa Marekani. Kwa sababu maamuzi na matamshi kama haya yatazidisha mara dufu tishio la nyuklia la Korea Kaskazini. Vilevile ni nchi gani itakayokubali kufanya mazungumzo na Marekani ambayo haiheshimu mapatano ya kimataifa?"

Katika upande mwingine mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Fedirica Mogherini amesema kuhusu hatua ya Trump ya kukataa kutangaza kwamba Iran imeheshimu makubaliano ya nyuklia kwamba: Makubaliano hayo ni mkataba wa pande kadhaa na kimsingi Marekani haiwezi kuvuruga makubaliano hayo.

Stratijia ya Rais wa Marekani kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na mismamo yake ambayo imetajwa kuwa si ya kidiplomasia, imepingwa pia na viongozi wa nchi za Ulaya. Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza imetangaza kuwa: Theresa May na viongozi wenzake wa Ujerumani na Ufaransa wametoa taarifa wakitangaza kuwa wataendelea kuheshimu na kutekeleza makubaliano ya JCPOA. Vilevile Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Boris Johnson amesema: JCPOA inazidisha amani ya dunia.

Mkurugenzi wa Muungano Dhidi ya Vita nchini Uingereza Lindsey Ann German anasema: Kimsingi Trump hakupasa kuwa Rais wa Marekani. Kiongozi huyo amehuisha tena ubaguzi na ukatili na matamshi yake dhidi ya makubaliano ya nchi kadhaa na Iran yameonesha kuwa, hawezi kusikilizana na yeyote. Donald Trump amedumisha siasa zake dhidi ya wanawake na kutishia jamii za waliowachache. Iran si tishio kwa nchi yoyote bali Trump ndiye mtu hatari sana na anaielekeza dunia katika machafuko na ukosefu wa amani".

Donald Trump

Siasa za Rais Dolad Trump wa Marekani zimeeneza hali ya hofu na ukosefu wa usalama duniani. Wataalamu wa masuala ya siasa wanasema kuwa, hakuna mtu anayeweza kutabiri au kuzatamia siasa za nje za Marekani zinakoelekea. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, Trump ameonesha kuwa ni mtu asiyetabirika na suala hilo linazidisha hali ya wasiwasi kuhusu usalama wa dunia.     

Tags

Oct 16, 2017 08:28 UTC
Maoni