• Clinton: Trump ameifanya Marekani ionekane nchi ya kijinga kuhusu Iran

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton amesema hatua ya Rais Donald Trump ya kuvuruga mapatano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 ni jambo ambalo limeifanya Marekani ionekane kuwa nchi duni na ya kijinga.

 

Siku ya Ijumaa Trump alizindua stratijia mpya ya Marekani kuhusu Iran ambapo alikataa kuidhinisha kuwa Iran inafungamana na mapatano ya nyuklia ambayo yanajulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelzwaji-JCPOA-. Mapatano hayo yalitiwa saini baina ya Iran na nchi za 5+1 ambazo ni Marekani, Uingereza, Ufaransa, Russia, China na Ujerumani. Nchi hizo zote isipokuwa Marekani zimetangaza kuwa Iran inafungamana na mapatano hayo.

Clinton na Trump

Katika mahojiano na CNN, Hilary Clinton amesema uamuzi wa Trump umepelekea hadhi ya Iran iimarike kwani Jamhuri ya Kiislamu haijakiuka mapatano hayo ya nyuklia. Amesema matamshi ya Trump yamepelekea Iran izidi kuimarika kimataifa huku Marekani ikionekana nchi yenye ujinga na duni.

Clinton aliyegombea kiti cha urais na Trump na kushindwa mwaka jana amesema uamuzi wa Trump wa kutoidhinisha mapatano ya nyuklia ya Iran ni kosa kubwa na ni jambo ambalo limepelekea Marekani isiweze kuaminika katika uga wa kimataifa.

 

Tags

Oct 17, 2017 04:23 UTC
Maoni