• Sheikh Naim Qassim: Trump ni mkiukaji wa ahadi na dhalimu

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon amejibu matamshi ya vitisho ya Rais Donald Trum wa Marekani ya kufuta makubaliano na Iran na kupasisha vikwazo vipya kwa kusema, kwa mtazamo wa wananchi wa Lebanon na wa mataifa mengine duniani, Trump ni mtu dhalimu na mkiukaji wa ahadi.

Sheikh Naim Qassim amesisitiza kuwa, Donald Trump anakabiliwa na maumivu na uchungu wa kushindwa Marekkani katika mafaili ya Mashariki ya Kati na hivi sasa anafanya njama za kuyatwisha mataifa ya Mashariki ya Kati siasa zake za utumiaji mabavu. 

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon amesema bayana kwamba, hadi sasa njama hizo za Marekani za kuyatwisha mataifa mengine siasa zake zimegonga ukuta na katu hazitafanikiwa.

Sheikh Naim Qassim ameongeza kuwa, uhalalishaji usio na msingi na uliojaa uongo wa Rais Trump kwa ajili ya kufuta makubaliano ya nyuklia kwa msingi kwamba, eti Iran haijafungamana na makubaliano hayo ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA unatolewa katika hali ambayo, Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA na nchi zote kubwa duniani zimesisitiza kwamba, Iran imeheshimu na kutekeleza kikamilifu makubaliano hayo.

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon sambamba na kusisitiza kwamba, siasa za Rais Trump sio hatari kwa wananchi wa Marekani tu bali ni tishio kwa walimwengu wote, amesema, Trump anafanya juhudi za kufidia kushindwa siasa zake katika Mashariki ya Kati na hawezi kuvumilia kabisa kuiona Iran yenye nguvu na iliyo imara.

Tags

Oct 17, 2017 04:24 UTC
Maoni