• Cairo watajwa kuwa mji hatari zaidi kwa wanawake duniani

Utafiti uliofanywa na Shirika la Thomson Reuters Foundation unaonyesha kuwa, jiji la Cairo ambao ndio mji mkuu wa Misri ndio mji hatari zaidi kwa wanawake kuishi duniani miongoni mwa miji mikubwa ulimwenguni.

Mji wa Karachi Pakistan umeshika nafasi ya pili katika orodha hiyo huku mji wa Kishasha wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ukishika nafasi ya tatu katika orodha ya miji hatari huku mji wa Lagos nchini Nigeria ukiwa ni wa nane kwenye orodha hiyo.

Jumla ya miji mikubwa  19 ililichunguzwa  ambayo ni miji yenye idadi ya watu inayofikia milioni kumi na zaidi.

Katika utafiti huo mji wa London umetajwa kuwa mji salama zaidi duniani kwa wanawake kutembea barabarani huku miji ya Tokyo na Paris ikishika nafasi ya pili na ya tatu.

Wanawake katika mitaa ya London Uingereza

Miongoni mwa yaliyozingatiwa kwenye utafiti huo ni unyanyasaji wa kingono, utamaduni unaowadhalilisha wanawake pamoja na upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wanawake, fedha na elimu.

Miongoni mwa wataalamu wa haki za wanawake waliombwa ushauri wakati wa kufanywa utafiti huo ni mwanahabari Shahira Amin, ambaye aliambia Thomson Reuters kwamba mambo yote kuhusu wanawake katika mji wa Cairo ni hatari. Hata kutembea tu barabarani, wanawake hunyanyaswa sana kwa maneno na vitendo.

Baadhi ya utafiti huo unaonyesha kuwa, katika mji wa Cairo Misri baadhi ya tamaduni za kale zimekuwa zikiwarejesha nyuma wasichana na kuwa kikwazo kwa maendeleo yao.

 

Oct 17, 2017 04:28 UTC
Maoni