• Moscow: Pendekezo la Marekani la kufanya kikao kuhusu Iran ni mzaha

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amelitaja pendekezo la Marekani la kutaka kuitishwa kikao maalumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na katika Kamati ya Haki za Binadamu kuhusu fujo za hivi karibuni nchini Iran kuwa ni mzaha.

Maria Zakharova amesema kuwa hakuna shaka kwamba ujumbe wa Marekani hauna maudhui muhimu za kuzungumzia. Zakharova ameongeza kuwa kwa mfano Nikki Haley Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa angeweza kuwahabarisha walimwengu kutoka kwa wafanya maandamano kuhusu tajiriba ya Marekani kuhusu kuwatia mbaroni kwa wingi raia wa nchi hiyo, kukandamizwa vikali harakati ya Wall Street  na kamatakamata ya kinyama iliyofanywa na eti askari usalama wa nchi hiyo katika mji wa Ferguson.  

Ukandamizaji wa kinyama wa polisi wa Marekani dhidi ya raia katika mji wa Ferguson nchini humo  

Raia wa Iran katika miji kadhaa hapa nchini wamekuwa wakifanya maandamano tangu Alhamisi iliyopita huku wakipiga nara wakilalamikia kutokuchukuliwa hatua za kushughulikia watu waliopoteza fedha zao katika taasisi za fedha, ughali wa baadhi ya bidhaa na usimamizi dhaifu wa serikali katika baadhi ya sekta. Hata hivyo wadandia fursa na wahalifu wanaoungwa mkono na baadhi ya nchi za Magharibi na Kiarabu na pia utawala wa Kizayuni walitumia vibaya maandamano hayo na kuyegeuza kuwa ghasia na fujo. 

Baada ya kujiri fujo hizo, Marekani imejitokeza na kutoa pendekezo la kufanyika kikao maalumu cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Kamati ya Haki za Binadamu kuhusu matukio yaliyojiri nchini Iran; ikiwa ni katika hatua yake ya kuingilia na kuwachochea wafanya fujo hapa nchini. 

Tags

Jan 03, 2018 07:45 UTC
Maoni