• Kim Jong-un: Vikwazo vya kimataifa dhidi ya Korea Kaskazini havina taathira yoyote

Kiongozi wa Korea Kaskazini amesema kuwa, hata kama vikwazo vya kimataifa dhidi ya Pyongyang vitaendelea kwa karne nzima, nchi yake haitokabiliwa na matatizo makubwa na badala yake itasimama kukabiliana na vikwazo hivyo.

Kim Jong-un amesema kuwa, moja ya sababu zinazoifanya Korea Kaskazini kupata ushindi ni uzingatiaji maalumu wa nchi hiyo kwenye ustawi wa elimu na teknolojia na kwa msingi huo ikiwa maadui wataweka vikwazo kwa miaka 10 au hata miaka 100, bado taifa hilo halitakumbwa na matatizo.

Kiongozi wa Korea Kaskazini

Ameongeza kwamba, uwezo mkubwa wa Pyongyang wa kukabiliana na mashinikizo ya kigeni unatonaka na kutofungamana kwake na upande wowote wa kigeni, kuwa na uchumi wa ndani wenye nguvu na pia kuwa na wataalamu waliobobea katika masuala ya utafiti na teknolojia.

Matamshi ya Kiongozi wa Korea Kaskazini yametolewa kutokana na vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutokana na miradi yake ya silaha za nyuklia na makombora yake ya balestiki. Hatua ya Pyongyang kufanya majaribio kadhaa ya silaha za atomiki na makombora ya balestiki mwaka jana, ilikabiliwa na ukosoaji mkubwa wa nchi kadhaa ikiwemo Marekani suala ambalo lilipelekea kuwekewa vikwazo vingine ikiwemo marufuku ya asilimia 90 ya kuingizwa mafuta nchini humo.

Baadhi ya silaha zinazoitia kiwewe Marekani na washirika wake

Hii ni katika hali ambayo hivi karibuni Rais Vladmir Putin wa Russia alinukuliwa akisema kuwa kiongozi huyo kijana wa Korea Kaskazini ni mwenye upeo mkubwa wa kiakili kama ambavyo pia amefanikiwa kumshindi hata Trump, Rais wa Marekani.

Tags

Jan 13, 2018 13:49 UTC
Maoni