Feb 09, 2018 04:34 UTC
  • Russia: Ushahidi unathibitisha Marekani inahamisha magaidi wa Daesh na kuwapeleka Afghanistan

Mjumbe Maalumu wa Rais wa Rassia katika Masuala ya Afghanistan amesema kuwa, Moscow ina ushahidi unaothibitisha kuwa, Marekani na Shirika la Kijeshi ya Nchi za Magharibi (NATO) zinahusika katika kuwahamisha magaidi wa Daesh kutoka Iraq na Syria na kuwapeleka Afghanistan.

Zamir Kabulov amesema NATO na Marekani zinadhibiti kikamilifu anga ya Afghanistan na kwamba aghlabu ya magaidi wa Daesh wanahamishiwa nchini humo kwa kutumia helikopta. 

Waziri wa Ulinzi wa Iran Amir Hatami pia amesisitiza ukweli huo katika mazungumzo yake ya jana na mwenzake wa Afghanistan, Tariq Shah Bahrami. Amir Hatami amesema kuwa, Marekani inataka kuwaokoa magaidi wa Daesh kutoka kwenye maangamizi ya Iraq na Syria kwa kuwahamishia nchini Afghanistan. 

Magaidi wa Daesh wanasaidiwa na Marekani na washirika wake

Taasisi mbalimbali za Afghanistan pia zimekuwa zikitahadharisha kuwa, Marekani inaendelea kuyaunga mkono na kuyasaidia makundi ya kigaidi hususan lile la Daesh kwa shabaha ya kuimarisha harakari za kundi hilo nchini humo.

Mwaka 2001 Marekani iliivamia Afghanistan kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na matunda pekee ya uvamizi huo hadi sasa ni ukosefu wa amani, ugaidi na kuongezeka uzalishaji wa mihadarati na dawa za kulevya nchini Afghanistan.   

Tags

Maoni