Feb 09, 2018 07:01 UTC
  • Russia: Mashambulio ya Marekani Syria ni jinai za kivita

Mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa ameyataja mashambulio ya anga ya Marekani katika mkoa wa Deir al Zor mashariki mwa Syria kuwa hayakubaliki na kwamba ni jinai za kivita.

Vasily Nebenzya amelalamikia mashambulio ya anga la Marekani huko mashariki mwa Syria na kueleza kuwa, Moscow ilishawaeleza viongozi wa Marekani kuwa kuwepo kwao huko Syria ni kinyume cha sheria na kwamba hakuna aliyevialika vikosi vya Marekani nchini Syria. Mwakilishi huyo wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa aliyasema hayo jana katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 

Vasily Nabenzya, mwakilishi wa kudumu wa Russia katika UN 

Nebenzya  ameongeza kuwa, viongozi wa Marekani wanasisitiza kuwa wanaendesha mapambano dhidi ya ugaidi huko Syria hata hivyo hadi sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa nchini humo dhidi ya ugaidi.

Wapiganaji  zaidi ya 100 waliotajwa kuwa na mfungamano na serikali ya Syria waliuawa jana Alhamisi katika mkoa wa Deir al Zor katika mashambulizi ya ndege za kivita za muungano eti wa kimataifa dhidi ya Daesh unaoongozwa na Marekani.  

Marekani na nchi kadhaa waitifaki wake zimeunda muungano eti dhidi kundi la kigaidi la Daesh tangu Agosti mwaka 2014 nje ya fremu ya Umoja wa Mataifa na pasina na kuwasiliana na serikali ya Syria. Muungano huo unaoongozwa na Marekani hadi sasa umeuwa raia wengi wasio na hatia katika mikoa ya Deir Zor, Raqqah na Aleppo huko kaskazini mwa Syria. 

Tags

Maoni