• Juhudi za Korea mbili za kuwa na mazungumzo ya viongozi wa ngazi ya juu

Katika hali ambayo mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi kali mjini Pyeongchang nchini Korea Kusini inayowashirikisha pia wanamichezo wa Korea Kaskazini ikiwa bado inaendelea, maafisa wa Korea mbili wanafanya juhudi kwa ajili ya kuwakutanisha viongozi wa mataifa hayo.

Katika uwanja huo, Lee Nak-yeon, Waziri Mkuu wa Korea Kusini amekutana na Kim Yoo-jung, Kiongozi Nambari Mbili wa Korea Kaskazini na kusisitiza kuwa, Korea mbili lazima zifanye juhudi za ziada za kuwakutanisha pamoja viongozi wa nchi hizo. Itakumbwa Ijumaa iliyopita na ikiwa ni baada kumalizika kwa vita kati ya Korea mbili yaani mwaka 1953, ujumbe wa ngazi za juu wa Korea Kaskazini ukiongozwa na Kim Jong-nam, Kiongozi Nambari Mbili wa nchi hiyo na kadhalika Kim Yo-jong, dada wa Kim Jong-Un, ulikutana na Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini kando na michuano ya msimu wa baridi kali inayoendelea hivi sasa nchini humo. 

Lee Nak-yeon, Waziri Mkuu wa Korea Kusini

Katika mazungumzo yao, Rais Jae-in aliutaka ujumbe wa Korea Kaskazini kufikisha mwaliko kwa Kim Jong-Un wa kutembelea Seoul, mji mkuu wa Korea Kusini. Michuano ya Olimpiki ambayo bado inaendelea mjini Pyeongchang nchini Korea Kusini, ni fursa ya kihistoria kwa ajili ya Korea mbili ambapo sambamba na wanamichezo na makundi ya wasanii maafisa wa ngazi za juu wa Korea Kaskazini nao walishiriki katika sherehe za ufunguzi, suala ambalo pia linaweza kuwa fursa kwa viongozi wa ngazi ya juu wa mataifa hayo kuweza kukutana. Suala la kukutana viongozi wa Korea mbili limejiri baada ya Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini kutoa mwaliko kwa Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini akimtaka kufanya safari mjini Pyongyang. Kadhalika safari ya ujumbe wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini nchini Korea Kusini na pia kukaribishwa vizuri na viongozi wa Seoul, inabainisha azma ya pande mbili ya kutatua mgogoro wao sambamba na kupanua wigo wa mahusiano yao.

Korea mbili

Hii ni kwa kuwa Seoul na Pyongyang zimefikia natija hii kwamba, mizozo na kuendelea na mivutano baina yao, si njia ya kumaliza mvutano uliopo katika Rasi ya Korea na badala yake inachochea zaidi fitina kati yao. Katika uwanja huo, Cheung Seong Chang mtaalamu wa masuala ya kisiasa wa taasisi ya Sejong ya mjini Seoul, Korea Kusini anasema: "Siasa kama vile za kuboresha mahusiano na Korea Kusini na pia kuanzisha anga ya mazungumzo kwa ngazi ya juu baina ya viongozi wa Korea mbili, inaweza kuandaa mazingira bora kwa ajili ya Korea mbili kuweza kuboresha mahusiano yao." Mwisho wa kunukuu. Pamoja na hayo kuendelea mahusiano na ushirikiano kati ya Seoul na Washington ni kizuizi kikuu katika kutekelezwa mapendekezo ya Korea Kaskazini na Korea Kusini ya kutatua mzozo kati yao.

Kiongozi wa Korea Kaskazini

Hii ni kwa kuwa hadi sasa Marekani imekuwa ikitekeleza siasa za kichochezi katika eneo la mashariki mwa Asia na Rasi ya Korea, siasa ambazo hata hivyo hivi sasa zinakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na mahusiano chanya yaliyoanza kujitokea kati ya Seoul na Pyongyang.

Layer Ball Bach mtaalamu wa masuala ya Korea Kaskazini katika Chuo Kikuu Huria cha Berlin, Ujerumani anasema: "Marekani inatumia stratijia ya mashinikizo na kutoa ahadi za matumaini lakini katika hilo hatujaiona ikifanya juhudi zozote za kutatua mzozo uliopo baina ya Korea mbili, na badala yake inazidi kuchochea mzozo tu katika eneo hilo."

Alaakullihal, hivi sasa dunia inasubiri kuona endapo viongozi wa Korea Kusini na Korea Kaskazini watakutana na hatimaye kupatikana usalama na utulivu katika eneo au la.

Tags

Feb 12, 2018 12:10 UTC
Maoni