• Carl Bernstein: Marekani haijawahi kuwa na Rais mwongo kama Donald Trump

Carl Bernstein, mwandishi wa habari wa Kimarekani amesema kuwa, katika historia yake Marekani haijawi kuwa na Rais mwongo kama Donald Trump.

Carl Bernstein ambaye anatambulika kutokana na kufichua kwake kashfa ya Watergate iliyopelekea kujiuzulu Richard Nixon Rais wa 37 wa Marekani amesema katika mahojiano aliyofanyiwa na Kanali ya Televisheni ya CNN kwamba, Marekani haijawi kupata Rais mwongo kama alivyo raia wa sasa wa nchi hiyo, Donald Trump.

Mwandishi wa habari huyo mtajika wa nchini Marekani amesema kuwa, uongo wa kila siku wa Donald Trump ni jambo ambalo linapaswa kukitia wasiwasi chama chake cha Republican.

Sambamba na kutilia shaka juu ya kujitokeza Donald Trump katika mazungumzo na Robert Mueller mwendesha mashtaka wa faili la uchunguzi kuhusu kuingilia Russia uchaguzi wa Marekani, Carl Bernstein amesisitiza kwamba, mpaka tutakapoona Trump amekaa na Mueller ndipo tutakapoamiani.

Rais Donald Trump wa Marekani

Amesema, hakuna kitu cha kutufanya tuamini kabla ya kutokea hilo hasa kutokana na mwenendo usioleweka wa Rais Donald Trump.

Carl Bernstein ameongeza kuwa, Trump ni mtu asiyeeleweka na daima amekuwa akiendelea kusema uwongo kuhusiana na mambo mbalimbali.

Serikali ya Russian imekuwa ikikanusha vikali taarifa za Marekani zinazodai kuwa iliingilia kati uchaguzi wa rais kumsaidia Donald Trump kushinda uongozi wa kipindi cha miaka minne katika ikulu ya White House, ikisisitiza kwamba, hazina msingi wowote, na ni madai yasiyo na maana.

Tags

Feb 13, 2018 02:57 UTC
Maoni