Feb 13, 2018 08:02 UTC
  • Korea Kaskazini: Trump na viongozi wengine wa Marekani wanaogopa silaha zetu za nyuklia

Serikali ya Korea Kaskazini imekitaja kitendo cha marekani cha kumwalika raia mmoja wa Korea Kaskazini aliyetoroka nchi sambamba na kusafiri naye baba wa mwanafunzi mmoja aliyefariki dunia kumpeleka katika michuano ya Olimpiki ya msimu wa baridi kali huko Korea Kusini kuwa kimetokana na woga wa Washington juu ya uwezo wa silaha za nyuklia wa Pyongyang.

Jana vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vilitangaza kwamba, hatua ya Trump ya kumwalika Ji Seong-ho, raia wa Korea Kaskazini ambaye kwa sasa anaishi nchini Korea Kusini na kumtaka ashiriki katika kikao cha hotuba yake ya mwaka nchini Marekani, au hatua ya Mike Pence, Makamu wa Rais wa Marekani ya kusafiri na Fred Warmbier, baba wa Otto Warmbier, katika michuano ya Olimpiki inayoendelea Korea Kusini, ni ishara kwamba Marekani imechanganyikiwa kutokana na uwezo wa silaha za nyuklia wa Pyongyang.

Kiongozi wa Korea Kaskazini kulia na Rais Donald Trump kushoto

Kadhalika ofisi ya Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa Jumatatu iliyopita, ilizitaja hatua mbili hizo kuwa ni 'zinaakisi kukata tamaa' kwa serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani. Inaelezwa kwamba, Otto Warmbier alifariki dunia baada ya kuachiliwa huru kutoka jela ya Korea Kaskazini kutokana na hali yake mbaya ya kiafya. Ji Seong-ho, alitoroka nchi mwaka 2006 na hadi sasa anaishi nchini Korea Kusini. 

Tags

Maoni